SIMBA YATOA TAMKO TUHUMA ZA HONGO KWA KABWILI
Uongozi wa klabu ya Simba SC, umeeleza kusikitishwa na kauli iliyotolewa na mlinda lango wa Yanga Ramadhani Kabwili akiituhumu klabu hiyo kuhusika na tukio la kupanga matokeo.
Taarifa iliyotolewa leo na Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo Senzo Mbartha imesema kuwa tuhuma hizo zinaichafua Simba, TFF pamoja na taswira ya mpira wa miguu nchini.
Amesema wana imani vyombo husika vitachukua hatua stahiki na wakati huohuo amelipongeza Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kwa kuanza uchunguzi wa tuhuma hizo mara moja.
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE