TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO IJUMAA YA JANUARY 31,2020
Klabu ya Tottenham ipo tayari kumuuza kiungo mkabaji raia wa Kenya Victor Wanyama, 28, kwa klabu yoyote itakayofikia dau la pauni milioni 8. Klabu ya Celtic imeonesha kuvutiwa kumsajili kiungo wake huyo wa zamani. (Mirror)
Manchester United wamepewa nafasi ya kumsajili kwa mkopo mshambuliaji Brazil Willian Jose, 28, kutoka klabu ya Real Sociedad. (Sky Sports)
Manchester United pia imefeli kumsajili mshambuliaji wa Bournemouth na Norway Joshua King, 28. (Telegraph)
Mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani, 32, hataihama klabu ya Paris St-Germain katika dirisha la usajili linalofungwa leo. (L'Equipe - in French)
Mshambuliaji wa Ujerumani Thomas Muller anaweza kuihama klabu yake ya Bayern Munich mwishoni mwa msimu huu. Mshambuliaji huyo mwenye miaka 30 amekuwa na klabu hiyo kwa kipindi chake chote cha uchezaji lakini kwa sasa hana raha kwa kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza. (Bild - in German)
Arsenal wanapanga kukamilisha usajili wa mkopo wa beki wa kulia wa Southampton na Ureno Cedric Soares, 28. (Standard)
Southampton hawataki kumuuza kiungo na kapteni wao raia wa Denmark Pierre-Emile Hojbjerg, 24, japo klabu ya Tottenham imeonesha nia ya kumtaka. (Star)
Klabu ya Lazio ya Italia inataka kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa na klabu ya Chelsea Olivier Giroud, 33. (Sky Sports)
Chelsea pia wanatarajiwa kupeleka ofa ya pili ya usajili kwa mshambuliaji wa Napoli na Ubelgiji Dries Mertens, 32, baada ya ofa ya kwanza kukataliwa. (Telegraph)
Kiungo mkabaji wa Serbia Nemanja Matic, 31, amegoma kuihama klabu ya Manchester United na yupo tayari kusaini mkataba mwengine wa kumbakisha Old Trafford. (Telegraph)
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE