Breaking News

MUONGOZO WA SERIKALI KWA MASHABIKI KUHUSU KURUHUSIWA KWENDA UWANJANI


KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dr.Hassan Abass amesema kuwa masuala ya michezo ambayo yameruhusiwa na Serikali kuanzia Juni Mosi yataendelea kama kawaida kama yalivyokuwa yakifanyika kabla ya janga la Virusi vya Corona.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, katika mkutano uliofanyika hivi karibuni, Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Dr. Abbas amesema kuwa Serikali imeridhia masuala hayo huku ikiwataka wadau kufuata kanuni zitakazotolewa kwa wadau wote.
Abbas amesema: “Rais wa Tanzania John Magufuli aliridhia michezo kuendelea nchini ambapo kuanzia Juni Mosi, shughuli za michezo nchini zitaendelea kwa sababu zilisimamishwa awali kutokana na janga la Virusi vya Corona.
Kuhusu Muongozo
Dr. Abbas alisema:-“28 Mei, Serikali ilitoa muongozo unaopaswa kuzingatiwa na wadau wa michezo ambao unapaswa ufuatwe, umetolewa na Wizara ya Habari pamoja na Wizara ya afya unaendelea kusambazwa kwa wadau mbalimbali.
Wahusika wa muongozo:-“Wadau wote wa michezo kuanzia viongozi, wachezaji, wadau, madaktri, wanapaswa wausome upo pia kwenye tovuti kwani unawahusu watu wote, maelekezo haya ni ya muhimu kuzingatiwa. Tumekaa na viongozi wote wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Baraza la Michezo Tanzania,(BMT) ,Bodi ya ligi na Wizara ya michezo ili waushushe kwa wadau wake.
Hiki hapa watakatana nacho watakaokiuka
 “Wale watakaokiuka adhabu itachukuliwa moja kwa moja bila kuwatazama usoni, tutazingatia muongozo tulioutoa.
Kuhusu Corona:-
“Pamoja na Virusi vya Corona kupungua ila ni lazima kuufuata muongozi kwani Corona bado ipo iwapo chama ama kikundi kitakiuka kitafungiwa.
Mtindo wa mechi utakuwa hivi:-
“Mtindo wa uendeshaji wa ligi husuani soka, awali kulikuwa na maoni kwamba ligi ichezwe kituo kimoja. Wengine walipendekeza ligi ichezwe nyumbani na ugenini. Sasa Serikali imeridhia mechi za ligi za soka zichezwe kama ilivyokuwa kabla ya Corona.
 “Yaani itakuwa nyumbani na ugenini hakutakuwa na vituo tena kama ilivyokuwa awali. Kwa sasa utaratibu ule wa nyumbani na ugenini utazingatiwa.
Kikomo cha mashabiki
“Ugonjwa umepungua hilo tunashukuru Mungu,  wagonjwa wamepungua, uamuzi wa Serikali kuhusu mashabiki, Serikali imeridhia mashabiki watakaotaka kwenda uwanjani wanaruhusiwa kwenda kwa taratibu zilezile za awali na kulipa kiingilio kama ilivyokuwa awali kabla ya Corona. Mashabiki watakaotaka na watakaokuwa na nafasi waende viwanjani.

Masharti ya mashabiki

“Lakini kila kiongozi anayehusika na eneo la viwanja anapaswa kuzingatia masharti yaliyowekwa ikiwa ni pamoja na viwanja vyote kuwa na sanitaiza, maji tiririka, kukaa mita moja, kuvaa barakoa kwa kila mtu, kunawa kwa sabuni na maji tiririka. Kanuni ya mita moja lazima izingatiwe na hili litasimamiwa na wadau wote. Hapa inatumika kanuni ya umma atakayekiuka katika hili hatua kali zitachukuliwa.

Kuhusu viwanja
 “Kila viwanja lazima kuwa na sceaning mashine mashabiki lazima wapimwe joto. Kwenye mechi ambazo ni kubwa tumeagiza kwamba wataingia mashabiki nusu katika mechi ambayo itakusanya mashabiki wengi.
Kuhusu timu zisizo na fedha
“Timu ambazo hazina fedha hilo ni jukumu lao kwani kuna fedha ambazo wanapewa kutoka kwa wadhamini wao ikiwa ni Vodacom, Azam TV na timu nyingine zina mdhamini mmojammoja hivyo wanapaswa watimize wajibu wao.
Msisitizo
“Serikali tunafahamu kwamba kuna michezo mingi sana na haya ni maelekezo ya jumla kwa kila mchezo.Serikali ya Tanzania inalinda afya za watanzania na inaamini kuwa katika hili wana michezo hawatatuangusha. Michezo ni afya na tunashukuru kwamba kila kitu kitakuwa sawa,” alimaziza Abbas.

Wallace Karia, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) alisema kuwa kikubwa ni shukrani kwa Serikali kwa kuruhusu masuala ya michezo kuanza na itakuwa fursa kwa kila mwanamichezo kufuata utaratibu ambao umewekwa.

Kuhusu wadhamini

“Wadhamini wetu wameendelea kuweka fedha ambazo walikuwa wanaweka kwani shughuli zilikuwa zinaendelea. Vilabu vimepewa hela na wadhamini ila hawasemi. Kwa kufanya hivyo wanachaguo lao iwe ni kushuka daraja na kuwaruhusu wengine wapande,” alisema.