Breaking News

TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO JUMANNE JUNE 02,2020

Mshindi mara sita wa tuzo ya Ballon d'Or Lionel Messi 32, atasalia Barcelona msimu ujao baada ya kipengele cha mkataba wake kinachomruhusu mshambuliaji huyo wa Argentina kuondoka baada ya mkataba kuisha msimu huu (Standard)

Liverpool wako kwenye majadiliano kuongeza mkataba wa kucheza kwa mkopo kwa kiungo Harry Wilsonv23, wa Bournemouth na mshambuliaji wa  Rhian Brewster 20, wa Swansea mpaka mwishoni mwa msimu (Telegraph)

Arsenal wako tayari kumpatia mchezaji wa nafasi ya ulinzi David Luiz 33, mkataba wa mwaka mmoja lakini watapunguza mshahara wake wa wiki (Mirror)

Kocha wa England Gareth Southgate hatahudhuria michezo ya Ligi Kuu England msimu utakapoanza kwa kuwa anahisi kuwa uwepo wake kwenye viwanja hauna umuhimu. (Star)

Chelsea imepeleka mapendekezo yake kwa Ligi Kuu England kuongeza idadi ya wachezaji wa kubadilisha wanaoruhusiwa kuwa kwenye benchi kuwa tisa badala ya saba katika kipindi hiki cha msimu uliobaki. (Mail)

Bayern Munich wanataka kumsajili winga wa Manchester City, raia wa Ujerumani Leroy Sane  24,na Kai Havertz 20, kutoka Bayer Leverkusen kama sehemu ya enzi mpya katika klabu, amesema Makamu Mwenyekiti. (Bayern1 via Evening Standard)

Chelsea inaiongoza Paris-St Germain katika kinyang'anyiro cha kumnasa beki wa kushoto wa Porto na raia wa Brazil Alex Telles 27. (Tuttosport via Express)

Chelsea wanafikiria kubadili uamuzi wao kwa kumsaini mshambuliaji wa RB Leipzig Timo Werner 24, ikiwa Mjerumani huyo ataonyesha nia utayari wa kuhama. (ESPN)

EPL kurejea tarehe 17 Juni
Real Madrid wamekataa nafasi ya kumsajili winga wa Chelsea Willian 31, kwa uhamisho huru.Mkataba wa mchezaji huyo wa Brazil unamalizika msimu huu. (Mirror)

Manchester United italipa pauni 10.5milioni  kwa ajili ya kuongeza mkataba wa kucheza kwa mkopo kwa mshambuliaji wa Nigeria Odion Ighalo mpaka mwezi Januari, ada ya pauni 6 milioni inakwenda Shanghai Shenhua na pauni 130,000 ni mshahara wa wiki. (Mail)