Breaking News

TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO IJUMAA JUNE 05,2020

Klabu ya Liverpool haitapambana na Chelsea kwa ajili ya kupata sahihi ya Timo Werner wakati mshambuliaji huyo 24, anayekipiga RB Leipzig yuko kwenye mpango wa kuelekea Stamford Bridge. (Evening Standard)

Manchester United wanajiandaa kutoa mkataba mpya kwa mchezaji wa nafasi ya ulinzi Brandon Williams ukiwa na marekebisho katika mshahara wake wa sasa wa pauni 40,000 kwa wiki, baada ya kufanya kazi nzuri msimu huu. (Athletic)

Arsenal wanaweza kuwa tayari kumuuza mchezaji wa nafasi ya ulinzi Kieran Tierney 23, kwa Leicester City, miezi 12 tu baada ya kuhamia Emirates(Express)

Tottenham wanamsubiri mchezaji wa nafasi ya ulinzi, Jan Vertonghen 33, kuamua kama ataendelea kubaki mpaka msimu utakapomalizika au ataondoka kabla msimu kuisha (Sky Sports)

Kiungo wa kati wa Newcastle Matty Longstaff hajakuwa mazoezini wiki hii wakati kukiwa hakuna uhakika kuhusu mustakabali wake kwenye klabu hiyo, huku klabu ya Udinese ya Serie A ikiripotiwa kutoa ofa ya  mshahara wa pauni 30,000 kwa wiki kwa mchezaji huyo, 20, ambaye mkataba wake utakwisha msimu huu. (Mail)

Manchester City wanatarajia kuanza mazungumzo na mchezaji raia wa  Hispania Eric Garcia huku klabu yake ya zamani Barcelona ikimtaka mchezaji huyo. (Mail)

Beki wa kushoto wa England Ben Chilwell 23, anashawishiwa  kujiunga na Chelsea baadae msimu huu lakini bado hajaomba kuondoka Leicester City . (Mirror)