TFF YAZIPIGA STOP SIMBA, YANGA, KMC FC, AZAM FC NA TRANSIT
Shirikisho la soka Tanzania TFF limetoa onyo kwa vilabu vya Simba SC, Yanga, KMC, Transit Cap na Azam FC kufuatia kucheza michezo ya kirafiki.
TFF limetoa katazo hilo na kutaka vilabu vitakavyotaka kucheza mechi za kirafiki lazima zionane nao kwanza, vilabu hivyo viliamua kucheza michezo ya kirafiki ili kujiweka fiti kuelekea kurejea kwa Ligi Kuu ambayo ilisimama sababu ya Corona.