Breaking News

YANGA KUJIPIMA NGUVU NA KMC

June 13 Klabu ya Yanga itaelekea mkoani Shinyanga kuumana na Mwadui FC katika mchezo wa kwanza baina ya timu hizo msimu ambao pia utakuwa ni wa ufunguzi wa ngwe ya lala salama Ligi kuu ya Vodacom.

Benchi la ufundi la Yanga chini ya kocha Msaidizi Charles Mkwasa walipendekeza kucheza mechi za kirafiki kujiweka sawa kabla ya kuanza kwa mikikimikiki ya Ligi.

Habari njema ni kuwa uongozi wa Yanga umethibitisha kuwa Klabu hiyo itashuka uwanja wa Uhuru Jumapili, June 07 kuumana na KMC FC.

Mkurugenzi wa mashindano klabu ya Yanga Thabiti Kandoro, amesema Yanga itajipima na wababe hao kutoka Kinondoni ikiwa ni sehemu ya program za Mwalimu kuiweka sawa timu kabla ya kwenda mkoani Shinyanga.

Amesema awali walikuwa na mpango wa kucheza angalau mechi mbili za kirafiki lakini kutokana na ufinyu wa muda, watacheza mchezo huo mmoja.