YANGA WABADILI GIA KWA MAKAMBO, KISA SIMBA
MKURUGENZI wa Uwekezaji ndani ya GSM, Injinia Hersi Said amesema kuwa mpango mkubwa wa kusajili wachezaji ndani ya Klabu ya Yanga kwa sasa ni kutowapa mikataba ya awali nyota wanaowahitaji wakihofia kupigwa bao na watani zao wa jadi Simba.
Injinia amesema kuwa awali walikuwa wakifanya hivyo kwa mastaa ambao walikuwa wanawahitaji mwisho wa siku wanawahiwa njiani kwa kupeleka mikataba yao kwa timu nyingine wakitaka waongezewe dau.
Miongoni mwa wachezaji ambao kwa sasa wapo kwenye rada za Yanga ni pamoja na Heritier Makambo ambaye alikuwa ndani ya Yanga msimu wa 2018/19 kwa sasa anakipiga Horoya.
"Hatuwezi kuwapa mikataba ya awali kwa sasa nyota ambao tunawahitaji kwa kuwa ni imekuwa ikiwapa faida wengine ambapo walikuwa wanapeleka mikataba hiyo kwa timu nyingine ili wapewe dau nono hilo hatutafanya kwa Makambo, tunaongea naye ila mkataba wa awali hatapewa," amesema.
Inaelezwa kuwa Simba wameanza kutazama mienendo ya Yanga ili waipige bao kwa nyota huyo ambaye alijenga urafiki na nyavu kwa kutupia mabao 19.

Chanzo: Championi