Breaking News

BAADA YA KUSUBIRIWA KWA MIEZI 7, DR CONGO YAPATA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI

Rais Felix Tshisekedi atangaza baraza jipya la mawaziri katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo hii leo Kinshasa, baada ya kusubiriwa kwa miezi saba.
Tshisekedi and Kabila
Katika serkali hiyo mpya, wanawake wamepewa asilimia kumi na saba ya mawiziri na wanaume asilimia 83. Mwandishi wa BBC Mjini Kinshasa anasema kuna sura mpya katika baraza hilo jipya la mawaziri ambazo hazijawahi kuwepo katika serikali.
Kadhalika kumeundwa wizara maalum ambayo itashughulikia watu wenye ulemavu. Serkali ya muungano ina jukumu la kuimarisha usalama nchini na kuboresha maisha ya raia wa DRCongo.
“Serikali hatimaye imewadia. Rais amesaini agizo rasmi na tutaanza kufanya kazi hivi karibuni,” shirika la habari la AFP limemnukuu waziri mkuu Sylvestre Ilunga.Kabila TshisekediAfter his inauguration, President Félix Tshisekedi (R) agreed to work predecessor Joseph Kabila (L)

Joseph Kabila avuna pakubwa

Mnamo Julai mwaka huu Rais wa DR Congo Felix Tshisekedi na mtangulizi wake Joseph Kabila walikubaliana kuunda serikali ya muungano.
Walikubali kuunda serikali itakayo kuwa na mawaziri 66. Kama walivyo kubaliana, chama cha rais huyo wa zamani sasa kimepata wizara 43, na kile cha rais Félix Tshisekedi kimejinyakulia wizara 23.
Maswali yaliulizwa wakati huo huku kukiwa na madai kwamba bwana Tshisekedi alifanya makubaliano ya kugawana mamlaka na bwana Kabila kabla ya uchaguzi huo.
Mashauriano yamekuwa yakiendelea kati ya vyama vyao na pande hizo mbili zilieleza kwamba mashauriano hayo yatapokamilika serikali itatangazwa.
Miezi sabaa baadaye hii leo sura mpya hiyo ya mawaziri, inayounda serikali ya Kinshasa imetangazwa rasmi.