Breaking News

WIMBO WA TETEMA WA RAYVANNY WAFUNGIWA NCHINI KENYA, SERIKALI YATOA SABABU

Wimbo wa Tetema ulioimbwa na msanii wa muziki kutoka Tanzania, Rayvanny umefungiwa kuchezwa nchini Kenya kwa madai kuwa una mashairi machafu ambayo yanaweza kuharibu jamii endapo wimbo huo utaendelea kuchezwa kwenye jamii.
Akitoa tamko hilo leo Jumanne Agosti 27, 2019, Mkurugenzi wa Bodi ya Filamu nchini humo, Dkt. Ezekiel Mutua amesema wimbo huo ni marufuku kupigwa kwenye mikusanyiko ya watu na badala yake utapigwa kwenye kumbi za starehe ambako wasikilizaji ni watu wakubwa.
Nyimbo za Tetema na Wamlambez ni marufuku kabisa kupigwa nje ya vilabu na Baa. Ni aibu kuona hata viongozi wa serikalini wakiimba na kucheza hadharani. Nyimbo ni chafu na haifai kwa matumizi ya umma, haswa watoto. Nyimbo zote zimejaa maudhui ya kingono. Ni muhimu kwa umma kujua kuwa ni chafu na haifai kupigwa kwenye jamii.“Ameandika Dkt. Mutua kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Wimbo mwingine uliofungiwa ni Walambez ulioimbwa  na kundi la Sailors la nchini humo.
Wimbo wa Tetema umetoka miezi 6 iliyopita na hadi sasa hivi, Umetazamwa mara Milioni 27 kwenye mtandao wa YouTube.