BABA ANUNUA NDEGE MBILI KWA BAHATI MBAYA AKITAFUTA ZAWADI YA BIRTHDAY YA MWANAE MTANDAONI
Baba mmoja nchini Saudi Arabia amenunua ndege mbili aina ya Airbus A350-1000 kwa bahati mbaya, wakati akitafuta zawadi ya Birthday ya mwanae mtandaoni.
Bilionea huyo anayefanya kazi katika Wizara ya Nishati nchini humo, amesema kuwa mtoto wake anapenda sana usafiri wa anga, Hivyo aliamua kumtafutia zawadi ya ndege za toy kwa ajili ya kuchezea.
Mwanaume huyo amesema alipoingia kwenye website ya Airbus alikutana na maswali kibao kwa lugha ya Kiingereza, jambo ambalo lilimchosha kwani hajui vizuri lugha hiyo.
Amesema alipojaribu kuangalia bei aliona imewekwa kwa mfumo wa Dola (USD), na aliona ni fedha ndogo ambayo kwenye akaunti yake alikuwa na uwezo wa kulipia.
Aliruhusu malipo ya awali kwa ajili ya kutengenezewa ndege hiyo.
Amesema baada ya miezi kadhaa kupita alipigiwa simu na kutumiwa email na watu wa Airbus, akiambiwa kuwa ndege zote mbili zipo tayari kinachohitajika ni rubani wa kuzisafirisha.
Tayari ndege zote mbili ameshazipokea na moja amemzawadia mtoto wake na moja ameiweka tu kwa matumizi ya familia.
Ndege aina ya Airbus A350-1000 inatajwa kuuzwa Bilioni 844.1 kwa ndege moja.