KAULI YA BASATA KUHUSU ‘TETEMA’ YA DIAMOND KUFUNGIWA KENYA
BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limeshangazwa na Serikali ya Kenya kuuzuia wimbo Tetema wa msanii kutoka Tanzania, Rayvanny, aliomshirikisha Diamond Platnumz kupigwa kwenye maeneo ya wazi nchini humo.
BASATA wamesema wimbo huo ni mzuri kwani hauna tatizo lolote na kawaida yao huwa wanakagua nyimbo zote na kama wimbo ukionekana una matatizo huwa wanachukua hatua ikiwemo kuufungia.
“Tumekuwa tukifuatilia nyimbo za wasanii wa hapa nchini na kuwaita wanapokosea. Tunatoa onyo na hata kufungia nyimbo zao, lakini huu (Tetema) hauna shida, ndiyo maana nasema sijui wametumia vigezo gani kuuzuia usichezwe mchana,” amesema Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza.
Wimbo wa Tetema umefungiwa na serikali nchini Kenya kutumika katika maeneo ya wazi kuanzia juzi Agosti 27, 2019, kwa madai kuwa una mashairi yanayoiharibu jamii, hususani watoto.
Usikubali kupitwa na chochote kile tembelea App hii kila mara kupata Habari zote zinazojiri Tanzania na nje ya Tanzania katika Mapenzi na Mahusiano, Elimu, Ajira, Michezo, Maisha, Siasa na Burudani.