SAMATTA USO KWA USO NA VIRGIL VAN DIJK
Chama cha soka ulaya leo kimechezesha droo ya kupanga makundi ya UEFA Champions League msimu wa 2019/2020, baada ya michezo ta Play off kumalizika.
UEFA wamepanga makundi nane huku nahodha wa Tanzania Mbwana Ally Samatta anayetarajiwa kuwa mtanzania wa kwanza kucheza UEFA Champions League, timu yake ya KRC Genk ya Ubelgiji imepangwa Kundi E na timu za Napoli, Liverpool pamoja na Salzburg.
Kupangwa huko ni wazi sasa Mbwana Samatta atakutana uso kwa uso na beki bora wa UEFA pamoja na mchezaji bora wa Ulaya Virgil van Dijk wa Liverpool baada ya kupangwa Kundi moja.
Usikubali kupitwa na chochote kile tembelea App hii kila mara kupata Habari zote zinazojiri Tanzania na nje ya Tanzania katika Mapenzi na Mahusiano, Elimu, Ajira, Michezo, Maisha, Siasa na Burudani.