Breaking News

MATOKEO YA SIMBA SC VS JKT TANZANIA AUGUST 29-2019

MABINGWA watetezi, Simba SC wameanza vyema msimu mpya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JKT Tanzania jioni ya leo Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Rwanda, Meddi Kagere alikaribia kufunga hat trick katika mechi ya kwanza baada ya kufunga mabao mawili, huku lingine likifungwa na Miraj Athumani ‘Madenge’ aliyerejeshwa kikosini msimu huu.

Kocha Mbelgiji, Patrick Aussems leo aliwaanzisha wachezaji wapta, Wabrazil Tairone Santos na Gerson Fraga kucheza pamoja safu ya ulinzi kwa mara ya kwanza tangu wasajiliwe Julai na wakafanya vizuri.


Kagere aliye katika msimu wake wa pili Msimbazi tangu asajiliwe kutoka Gor Mahia ya Kenya, alifunga bao la kwanza sekunde ya 20 ya dakika ya kwanza akimalizia pasi ya kiungo Hassan Dilunga kabla ya kufunga la pili dakika ya 58 akimalizia pasi ya kiungo mwingine mzawa, Muzamiru Yassin.

Kagere alikaribia kukamilisha hat trick dakika ya 65 kama si shuti lake kugonga mwamba – lakini dakika 73 akamtilia krosi nzuri mtokea benchi Miraji Athumani 'Madenge' aliyefunga kwa kichwa kuipatia Simba SC bao la tatu.

Edward Songo aliyetokea benchi pia akaifungia bao la kufutia machozi JKT Tanzania dakika ya 87 kwa shuti la umbali wa mita 25 lililompota kipa namba wa Simba na timu ya taifa ya Tanzania, Aishi Salum Manula.

Usikubali kupitwa na chochote kile tembelea App hii kila mara kupata Habari zote zinazojiri Tanzania na nje ya Tanzania katika Mapenzi na Mahusiano, Elimu, Ajira, Michezo, Maisha, Siasa na Burudani.