PSG YAONYESHA JEURI, YAKATAA PAUNI MILIONI 118 NA WACHEZAJI WATATU + DEMBELE KUTOKA BARCELONA, MADRID YAJARIBU ZALI
Paris Saint-Germain imekataa ofa kutoka Barcelona kwaajili ya kumsajili Neymar baada kukaa kikao cha siku mbili bila mafanikio.
Dirisha la usajili barani Ulaya linatarajiwa kufungwa siku ya Jumatatu ijayo, Barca imejaribu kufanya kila linalowezekana ili kumsajili nyota huyo wa Brazil.
Kwa mujibu wa gazeti la michezo la Mundo Deportivo, Barca iliandaa ofa ya pauni milioni 118 pamoja na wachezaji watatu ambao ni Ivan Rakitic, Jean-Clair Todibo na mmoja kwa mkopo Ousmane Dembele hata hivyo imekataliwa na matajiri hao wa Ufaransa.
Na kwa upande wa RMC Sport limeripoti kuwa jitihada za Barcelona hazikutosha kwa PSG kumuachia Neymar ambaye wanaamini thamani yake ni kubwa mno baada ya kumnunua miaka miwili iliyopita kwa dau lililovunja rekodi ya zaidi ya pauni milioni 198.
Baadhi ya vyombo vya habari kutoka Hispania vimeripoti kuwa mahasimu wa Barcelona ambao ni Real Madrid wapo kwenye nafasi ya kumwania nyota huyo kabla ya dirisha la usajili kufungwa.
Neymar ambaye bado hajaanza kuitumikia PSG msimu huu, hajaanza mazoezi kufuatia kusumbuliwa na majeruhi yaliyompelekea kuikosa michezo ya Copa America.
Usikubali kupitwa na chochote kile tembelea App hii kila mara kupata Habari zote zinazojiri Tanzania na nje ya Tanzania katika Mapenzi na Mahusiano, Elimu, Ajira, Michezo, Maisha, Siasa na Burudani.