Breaking News

IBRAHIMOVIC ATAMANI KUREJEA MAN UNITED

Mshambuliaji wa LA Galaxy Zlatan Ibrahimovic amesema yupo tayari kurejea klabu yake ya zamani ya Manchester United mwezi Novemba. 
Mshambuliaji huyo mkongwe mwenye miaka 37 amepachika magoli 46 katika michezo 49 toka alipohamia kwenye ligi ya Marekani (MLS) mwezi Machi 2018. “Ninaweza kucheza kwa urahisi kabisa katika Ligi ya Primia.
Hivyo, kama United watanihitaji, nipo tayari,” amesema. Ibrahimovic aliifungia Man United magoli 28 msimu wa 2016-17 kabla ya kuandamwa na majeraha ya goti.
Mkataba wake wa miaka miwili na klabu ya United ulivunjwa kwa pande zote mbili kuridhia na kumruhusu kwenda Marekani. Hata hivyo, endapo atafanikiwa kurejea United, atalazimika kusubiri mpaka mwezi Januari ambapo dirisha la usajili kwa ligi ya Uingereza litafunguliwa.
Zlatan Ibrahimovic
Image captionIbrahmovic alishinda Kombe la Ligi, Ngao ya Jamii na Kombe la Europa akiwa na Man Utd
“Nimefanya kazi yangu Ulaya. Niliifurahia, nina mataji 33 ambayo nimeyashinda kule, na ninaamini nitashinda kitu hapa. “Baada ya hapo tutaona nini kitafuata na safari itaishia wapi.”
Ibrahimovic amesema kuwa anaendelea kuangalia mechi za Manchester United na kusisitiza kuwa walikosa bahati walipofungwa na Crystal Palace Jumamosi. Marcus Rashford alikosa penati wakifungwa na Palace, kama ilivyotokea kwa Paul Pogba wakati wa sare na Wolves siku tano kabla.
Video Player
00:00
00:00
“Nimeangalia mchezo wa mwisho na naamini hawakuwa na bahati tu,” amesema. “Kama wakipata penati unakuwa mchezo wa tofauti kabisa, lakini mchezo nchini England hukamilika pale tu kipyenga cha mwisho kinapolia. “Kitu chochote kinaweza kutokea, hususani katika dakika za mwisho wakati joto hupanda kweli kweli.” Ibrahimovic pia amebainisha kuwa yungali anawasiliana na Pogba ambaye amekuwa akihusishwa na harakati za kutaka kuihama klabu hiyo. “Naongea nae. Namshauri sana – lakini iwezi kuwambia nyinyi! (waandishi)” alimalizia.

Usikubali kupitwa na chochote kile tembelea App hii kila mara kupata Habari zote zinazojiri Tanzania na nje ya Tanzania katika Mapenzi na Mahusiano, Elimu, Ajira, Michezo, Maisha, Siasa na Burudani.