TRUMP KUKUTANA NA RAIS WA IRAN
Rais wa Marekani Donald Trump amesema yuko tayari kukutana na rais wa Iran Hassan Rouhani chini ya makubaliano sahihi.
Maamuzi hayo yanakuja mara baada ya waziri wa mambo ya nje alipofanya ziara fupi bila kutangaza katika mkutano wa matifa makubwa 7 yenye nguvu duniani siku ya jumapili.
Mahusiano kati ya Iran na Marekani yamezidi kuwa mabaya tangu Washington ilipojitoa mwaka jana katika makubaliano ya mwaka 2015 ya kudhibiti matumizi ya nyuklia ya Iran.
Licha ya kwamba, siku ya Jumatatu Trump alisema kwamba ana matumain chanya juu ya matarajio ya mpango mpya wa nyuklia na Iran .
“Iran sio nchi ileile miaka miwili na nusu iliyopita wakati nilipoingia madarakani,” aliwaambia waandishi wa habari katika mkutano wa G7 akiwa na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron .
“Nina imani kuwa Iran litakuwa taifa zuri… lakini hawapaswi kuwa na silaha za nyuklia,” alisema,” lazima kuwa lazima wawe wachezaji wazuri kabla hajakubali katika mkutano.
Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Mapema siku ya jumatatu, bwana Rouhani alisema kuwa yuko tayari kukutana na yeyote kama ataona kuwa itakuwa ni kwa manufaa ya Iran.
“Kama sina uhakika kuwa kuhudhuria mikutano hiyo hakutasaidia kuendeleza nchi yangu au kutatua matatizo ya watu wa nchi basi sitasita kufanya hivyo,” alisema.
Trump alitoa hotuba ya kuhitimisha mkutano wa G7- mkutano ulioudhuriwa na viongozi kutoka Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan, Uingereza na Marekani.
Masuala mengine yaliyojadiliwa ni pamoja na moto wa Amazon , maendeleo ya Ukraine, Libya na Hong Kong.