WANAFUNZI 300 WAPATA UJAUZITO MWANZA, WADAIWA KURUKA UKUTA USIKU
Kutokana na ripoti ya sekta ya elimu kwa Mkoa wa Mwanza imeonyesha kuwa mwaka 2018 jumla ya wanafunzi 300 wa shule za msingi na Sekondari walipata ujauzito huku kesi nyingi zikionekana kuishia vituo vya polisi na ofisi za kata.
Pia ripoti hiyo imebainisha kwamba baadhi ya wanafunzi wanaoishi shule za bweni wamekuwa na tabia ya kutoroka usiku na kuwafuata wanaume uraiani ambapo baadhi yao wamekutawa na simu zinatumika katika mawasiliano ya mapenzi.
Akiwasilisha ripoti hiyo juzi katika kikao cha semina ya iliyohusishana kamati ya mkoa ya ulinzi wa wanawake na watoto na Shirika la la Kutetea Haki za Wanawake na Watoto (Kivulini), Ofisa Elimu Taaluma Mkoa wa Mwanza, Jovitha Mwombeki alisema ripoti hiyo ni ya halmashauri nane za mkoa huo. Alifafanua kuwa kwa upande wa shule za msingi, wanafunzi waliopata ujauzito wakiwa shuleni ni 49 ambapo Ilemela zilikuwa mbili, Kwimba 11, Magu 26, Jiji la Mwanza 3, Sengerema 9, Ukerewe 9, Buchosa na Misungwi hakiwa na matukio hayo.
Mwombeki alisema upande wa Sekondari mimba zilikuwa 251 ambapo Buchosa 23, Ilemela 2, Kwimba 42, Magu 17, Misungwi 98, Jiji la Mwanza, 36, Ukerewe 32 huku Sengerema haikupata tukio la mimba. “Katika kukabiliana na suala hili la ujauzito kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, hatua mbalimbali zimechukuliwa kwa walioshiriki kuwapatia mimba hawa watoto wetu, mfano Buchosa kuna matukio 23 ya msingi na sekondari ambapo kesi zote zipo polisi, Ilemela kuna mimba tano na kesi zote zipo polisi.
“Kwimba kuna mimba 53 ambapo kesi 37 zipo polisi, 10 zipo mahakamani na sita zipo kwa watendaji wa kata wakiendelea kuchunguza na kuwatafuta watuhumiwa, upande wa Magu jumla ya mimba 43 na zote zipo kwa watendaji wa kata, Misungwi ni mimba 98 na kati ya hizo 54 zipo polisi, 37 mahakamani na tano zimehukumiwa. “Mwanza jiji kuna jumla ya mimba 39 na zote zipo kwa watendaji wa kata wakiwatafuta watuhumiwa, Sengerema kesi za mimba zipo tisa ambapo zote zipo polisi na Wilaya ya Ukerewe mimba ni 41 na zote zipo polisi,”alisema.
Chanzo Mtanzania digital
Usikubali kupitwa na chochote kile tembelea App hii kila mara kupata Habari zote zinazojiri Tanzania na nje ya Tanzania katika Mapenzi na Mahusiano, Elimu, Ajira, Michezo, Maisha, Siasa na Burudani.