KESI INAYOMKABILI HAJI MANARA NA WENZAKE WATATU YASOGEZWA MBELE
Kesi ya madai inayomkabili Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara na wenzake watatu katika Mahakama ya Mkazi Kisutu jijini Dar Es Salaam, imeahirishwa hadi Septemba 30, 2019.
Haji Manara na wenzake wawili Beatrice Ndungu na Palm General Supply wanadaiwa fidia ya Tsh Milioni 83.3 na mfanyabiashara Abu Masoud Al Jahdhamy.
Imeelezwa kuwa watatu hao walipokea bidhaa zenye nembo ya Dela Boss Perfume bila kuzilipia.
Kesi hiyo ya madai yenye namba 128/2019 imeahirishwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Agostina Mbando mpaka tarehe 30 mwezi ujao Mwaka huu itakapotajwa tena.
Usikubali kupitwa na chochote kile tembelea App hii kila mara kupata Habari zote zinazojiri Tanzania na nje ya Tanzania katika Mapenzi na Mahusiano, Elimu, Ajira, Michezo, Maisha, Siasa na Burudani.