Breaking News

WATOTO MAPACHA WALIOUNGANA WATENGANISHWA, WAREJEA NCHINI – VIDEO

Hakika Mungu ni muweza… hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya watoto mapacha waliozaliwa wakiwa  wameungana na hatimaye kwenda kufanyiwa upasuaji wa kutenganishwa nchini Saudi Arabia, Almenesia na Ainisia Beatus wamewasili nchini wakiwa tayari wametenganishwa.

Watoto hao waliozaliwa mkoani Kagera na na kwenda kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha King Abdullah mjini Riyadh, kwa ufadhili wa Mfalme wa Saudi Arabia, ambapo gharama za matibabu yao ni zaidi ya dola za Kimarekani 5,000, wamewasili leo Ijumaa, Agosti 30, 2019, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.
Usikubali kupitwa na chochote kile tembelea App hii kila mara kupata Habari zote zinazojiri Tanzania na nje ya Tanzania katika Mapenzi na Mahusiano, Elimu, Ajira, Michezo, Maisha, Siasa na Burudani.