Breaking News

AZAM YATOA TIKETI 500 BURE KUISAPOTI STARS


LEO timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stasr itashuka uwanjani kumenyana na timu ya Taifa ya Burundi kwenye mchezo wa kusaka tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia linalotarajiwa kufanyika nchini Quatar mwaka 2022.

Mashabiki 500 tayari wana tiketi zao za bure ambazo wamepewa na uongozi wa timu ya Azam FC.

Tiketi hizo zilitolewa jana uwanja wa Chamazi wakati Azam FC ikicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Pan Africans hivyo wana uhakika wa kulea shangwe zote uwanja wa Taifa.

Uongozi wa Azam FC umesema kuwa lengo kubwa la kufanya hivyo ni kuipa sapoti timu ya Taifa ya Tanzania.

Mchezo wa kwanza uliochezwa nchini Burundi Stars ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 hivyo leo wanahitaji ushindi ili kusonga mbele.

Usikubali kupitwa na chochote kile tembelea App hii kila mara kupata Habari zote zinazojiri Tanzania na nje ya Tanzania katika Michezo, Magazeti, Mahusiano, Elimu, Ajira, Video, Audios, Tamthilia na Udaku.