Breaking News

DE GEA WA YANGA KIMEELEWEKA CAF


Rasmi kipa namba moja wa Yanga, Farouk Shikalo 'de Gea' atakuwa sehemu ya kikosi cha kwanza kitakachoivaa Zesco ya nchini Zambia baada ya juzi usiku kupokea kibali.

Yanga itaavana na Zesco Septemba 14, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kabla ya kurudiana wiki mbili zijazo huko Zambia katika mchezo wa Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kipa huyo na wachezaji wengine wawili walikosa michezo miwili ya michuano hiyo walipocheza na Township Rollers ya Botswana ambao ni David Molinga na Seleman Moustafa kutokana na kukosa vibali.

Mratibu wa timu hiyo, Hafidh Saleh alisema kuwa ni habari njema kwa mashabiki wa Yanga kipa wao atakuwepo uwanjani katika mchezo wao dhidi ya Zesco.

Hafidh alisema kuwa tayari kipa huyo amepewa taarifa mara baada ya kumalizika kwa mchezo wao wa kimataifa anatakiwa kuwahi nchini kwa ajili ya kuwahi maandalizi ya mchezo huo mgumu watakaoanza nao nyumbani.

Aliongeza kuwa kupata kibali kwa kipa huyo kutaimarisha kikosi chao kinachoundwa na wachezaji wengi wazuri watakaowapa matokeo kwenye mchezo huo.

“Ni kweli Shikalo pekee ndiye aliyepata kibali kutoka Caf kitakachomruhusu kucheza mchezo wetu dhidi ya Zesco tutakaoanza kucheza hapa nyumbani ambao tunahitaji ushindi.

“Hiyo ni habari njema kwea mashabiki wetu kuwa watarajie kuona mabadiliko makubwa katika kikosi chao kitakachocheza na Zesco.

“Molinga na Selemani (Moustafa) wenyewe bado hawajapata kibali Caf, hiyo ni baada ya usajili wao kuchelewa kufika Caf, lakini upo uwezekano wa kuwepo kucheza katika hatua ya makundi,” alisema Hafidh.

Usikubali kupitwa na chochote kile tembelea App hii kila mara kupata Habari zote zinazojiri Tanzania na nje ya Tanzania katika Michezo, Magazeti, Mahusiano, Elimu, Ajira, Video, Audios, Tamthilia na Udaku.