Breaking News

JIMY KINDOKI AULA YANGA

Uongozi wa klabu ya Yanga, umemteua Jimmy S Msindo "jimmy kindoki" kuwa mjumbe wa kamati ya hamasa ya klabu hiyo kuanzia tarehe 05/09/2019.

Kazi za jimmy kindoki katika klabu ya Yanga SC zitakuwa kama ifuatavyo:

1.Kushauri kamati ya utendaji na kujenga mikakati ya njinsi ya kujenga ,kuleta na kuendeleza hamasa ya wanachama wa klabu ya Yanga SC.

2.Kuhamasisha timu zote za klabu ya Yanga ili zifanye vyema katika mashindano yote.

3.Kuwahimiza wanachama wa klabu hiyo kuhudhuria kwa wingi katika kila Yanga ichezapo.

4.Kuhamasisha wapenzi wa klabu kuwa wanachama kamili wa klabu hiyo.

5.Kuhamasisha wanaYanga kushiriki kwenye shughuli zote zinazo ihusu klabu hiyo.

Usikubali kupitwa na chochote kile tembelea App hii kila mara kupata Habari zote zinazojiri Tanzania na nje ya Tanzania katika Michezo, Magazeti, Mahusiano, Elimu, Ajira, Video, Audios, Tamthilia na Udaku.