Breaking News

KAA TAYARI KWA UJIO WA ‘MICROBIAL FUEL CELL’ TEKNOLOJIA YA KUCHAJI SIMU KWA KUTUMIA MKOJO

Mwaka 2013, Wanasayansi kutoka Uingereza waligundua teknolojia ya kuzalisha umeme kwa kutumia mkojo wa binadamu itwaayo ‘Microbial Fuel Cells’ (MFC), Hatimaye mitambo hiyo tayari imeboreshwa na ipo mbioni kuingia sokoni.
Watafiti hao ambao wanatoka katika maabara kubwa nchini Uingereza ya Bristol Robotics, Wamesema kuwa ugunduzi huo utasaidia zaidi sehemu ambazo hazijafungwa umeme ikiwemo milimani na maeneo yenye barafu.
Kifaa hicho cha Microbial Fuel Cell hutumia bakteria wa kwenye mkojo na kuchuja chembechembe zote zinazopatikana na kubakiza elekroni maalum ambazo hubadilishwa kuwa umeme kwaajili ya matumizi.
Imeelezwa kuwa Lita mbili za mkojo zina uwezo wa kuzalisha nguvu ya umeme ya kiasi cha milliwati 40-60, Ambazo zinaweza kuchaji simu na kuwasha vifaa vingine vinavyotumia umeme.
Kwa mujibu wa mtandao wa Tech Crunch, Mashine hizo huenda zikaingia sokoni mwishoni mwa mwaka huu.

Usikubali kupitwa na chochote kile tembelea App hii kila mara kupata Habari zote zinazojiri Tanzania na nje ya Tanzania katika Michezo, Magazeti, Mahusiano, Elimu, Ajira, Video, Audios, Tamthilia na Udaku.