Breaking News

KAULI YA ZAHERA KUELEKEA MCHEZO VS ZESCO

Baada ya kufanya maboresho katika App yetu sasa tunakuomba ufanye ku update ili kuendelea kupata habari zetu zote pamoja na kutazama mechi live, kusikiliza radio zote za Tanzania na mengine mengi katika ubora zaidi

ILI KU UPDATE BOFYA👉👉👉 HAPA 
HAKIKISHA UMEUPDATE


Licha ya kocha wa Zesco United, George Lwandamina kutamba kuwa timu yake haijawahi kufungwa katika uwanja wake wa nyumbani tangu mwaka 2014, kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema watakuwa timu ya kwanza kushinda nchini Zambia.

Akizungumza jana muda mfupi kabla ya kukwea pipa kuelekea Zambia, Zahera alisema wanahitaji kushinda kwa bao 1-0 tu ili waweze kutinga makundi.

"Kule Zambia tunahitaji bao moja tu ili kuingia hatua ya makundi, hatuna shida ya kufunga mabao 100 tukipata moja tu litatutosha na kutuvusha hatua hii," alisema

Aidha Zahera amesema wamejiandaa kikamilifu wakiwa wamefanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza kwenye mchezo wa kwanza.

Zahera aliondoka asubuhi akiwa na wachezaji 10 katika msafara wa kwanza wa timu hiyo.

Wachezaji waliobaki pamoja na viongozi wengine wa benchi la ufundi waliondoka saa mbili usiku wa jana Jumanne.

Zaidi Na Zaidi Tembelea App Hii Kila Mara , Kila Saa Kupata Habari Zote Zinazojiri Tanzania Na Nje Ya Tanzania Katika Mapenzi Na Mahusiano, Elimu, Ajira, Michezo, Maisha, Magazeti, Videos, Audios, Tamthilia Na Burudani.