Breaking News

MASHABIKI WAISHAMBULIA NYUMBA YA NAHODHA TIMU YA TAIFA KISA PENATI


Mashabiki jijini Free Town wamevamia na kushambulia kwa mawe nyumba ya Nahodha wa timu ya soka ya Sierra Leone, Umaru Bangura.

Mashabiki hao walifanya hivyo wakidai wamechukizwa na yeye kukosa penalti katika mechi ya kuwania kufuzu kucheza Kombe la Dunia 2022.

Bangura amelaani kitendo hicho na kusema nusura auvue unahodha kwa kuwa hawakumtendea haki.

Pamoja na hivyo, nyota huyo anayekipiga nchini Uswiss amesema amelazimika KUBAKI chumbani kwa kuwa ana hofu na maisha yake.

Usikubali kupitwa na chochote kile tembelea App hii kila mara kupata Habari zote zinazojiri Tanzania na nje ya Tanzania katika Michezo, Magazeti, Mahusiano, Elimu, Ajira, Video, Audios, Tamthilia na Udaku.