Breaking News

YANGA DIMBANI LEO VS TOTO AFRICANS


Klabu ya Yanga leo Jumanne itashuka kwenye uwanja wa Nyamagana mkoani Mwanza kucheza na timu ya Toto Africans ukiwa ni mchezo wa kirafiki.

Yanga iko mkoani Mwanza kujiandaa na mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya ZESCO United ambao utapigwa Jumamosi Septemba 14 kwenye uwanja wa Taifa.

Baada ya juzi kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Pamba FC, leo mabingwa hao wa kihistoria watakamilisha ratiba yao ya michezo ya kirafiki mkoani Mwanza.

Usikubali kupitwa na chochote kile tembelea App hii kila mara kupata Habari zote zinazojiri Tanzania na nje ya Tanzania katika Michezo, Magazeti, Mahusiano, Elimu, Ajira, Video, Audios, Tamthilia na Udaku.