Breaking News

MATOKEO YA TANZANIA BARA U20 DHIDI YA ETHIOPIA

Baada ya kufanya maboresho katika App yetu sasa tunakuomba ufanye ku update ili kuendelea kupata habari zetu zote pamoja na kutazama mechi live, kusikiliza radio zote za Tanzania na mengine mengi katika ubora zaidi

ILI KU UPDATE BOFYA👉👉👉 HAPA 
HAKIKISHA UMEUPDATE

Timu ya Taifa ya Tanzania Bara imeanza vyema michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 20 Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Challenge U20) baada ya ushindi wa 4-0 dhidi ya Ethiopia leo mjini Jinja, Uganda.

Nyota wa mchezo wa leo alikuwa ni chipukizi wa akademi ya Azam FC aliyekuwa kwa mkopo Coastal Union ya Tanga, Andrew Albert Simchimba aliyefunga mabao matatu peke yake dakika za 38, 49 na 85, baada ya chipukizi mwingine, Kelvin Pius John aliye mbioni kusajiliwa KRC Genk ya Ubelgiji kufunga la kwanza dakika ya 18.

Bara inayofundishwa na kocha wa Mtibwa Sugar ya Morogoro, Zubery Katwila itarudi uwanjani Jumanne kumenyana na Kenya kabla ya kukamilisha mechi zake za Kundi B kwa kucheza na ndugu zao, Zanzibar Septemba 26.
Chipukizi Andrew Simchiba akishangilia na wenzake baada ya kuifungia Bara mabao matatu leo
Mfungaji wa bao la kwanza la Bara, Kelvin Pius John (kulia) akiwania mpira dhidi ya beki wa Ethiopia

Hatua ya Robo Fainali itafuatia Septemba 29, Nusu Fainali Okatoba 2 na Fainali ya michuano ya CECAFA Challenge U20 mwaka 2019 itapigwa Oktoba 5.

Zaidi Na Zaidi Tembelea App Hii Kila Mara , Kila Saa Kupata Habari Zote Zinazojiri Tanzania Na Nje Ya Tanzania Katika Mapenzi Na Mahusiano, Elimu, Ajira, Michezo, Maisha, Magazeti, Videos, Audios, Tamthilia Na Burudani.