MATOKEO YA TANZANIA VS SUDAN SEPTEMBER 22,2019
Baada ya kufanya maboresho katika App yetu sasa tunakuomba ufanye ku update ili kuendelea kupata habari zetu zote pamoja na kutazama mechi live, kusikiliza radio zote za Tanzania na mengine mengi katika ubora zaidi
ILI KU UPDATE BOFYA👉👉👉 HAPA
HAKIKISHA UMEUPDATE
Timu ya Taifa ya Tanzania imejiweka katika mazingira magumu ya kufuzu Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) mwakani nchini Cameroon baada ya kufungwa 1-0 nyumbani leo na Sudan katika mchezo wa kwanza wa raundi ya pili na ya mwisho ya mchujo kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, bao lililoizamisha Tanzania limefungwa na Yasir Mohamed katika dakika ya 60 akimalizia mpira uliogonga mwamba baada ya krosi iliyopigwa na Ranadan Agab baada ya kumtoka beki Boniphace Maganga upande wa kuliaa.
Sasa Tanzania wanatakiwa kwenda kushinda 2-0 ugenini kwenye mchezo wa marudiano ambao Sudan wameomba ufanyike Jijini Kampala, Uganda October 18 kwa sababu ya machafuko yanayoendelea nchini mwao.
Sudan inayofundishwa na kocha wa zamani wa klabu ya Simba ya Dar es Salaam, Mcroatia Zdravko Logarusic walipata pigo kwenye dakika ya 32 baada ya kiungo wake Mohammed Alrashed kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo, nafasi yake ikichukuliwa na Nazar Hamid.
Pamoja na kufungwa katika mchezo huo, Taifa Stars inayofundishwa na kocha Mrundi, Etienne Ndayiragije ilicheza vyema na kutengeneza nafasi kadhaa, lakini kwa mara nyingine tena tatizo likawa katika umaliziaji.
Peke yake, mshambuliaji aliyerejea Azam FC ya nyumbani baada ya msimu mmoja wa kuwa na Tenerife nchini Hispania alipoteza nafasi nzuri za kufunga dakika ya saba, 19 na 85.
Zaidi Na Zaidi Tembelea App Hii Kila Mara , Kila Saa Kupata Habari Zote Zinazojiri Tanzania Na Nje Ya Tanzania Katika Mapenzi Na Mahusiano, Elimu, Ajira, Michezo, Maisha, Magazeti, Videos, Audios, Tamthilia Na Burudani.