RC MAKONDA AMZAWADIA KASEJA TSH. MILIONI 10
Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeinga hatua ya makundi ya kuwania tiketi ya kufuzu fainali za kombe la dunia nchini Qatar mwaka 2022.
Mara baada ya Mchezo huo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa atampatia Mlinda Mlango wa Taifa Stars Tsh. Milioni 10.
Katika mchezo huo Mlinda Mlango Juma Kaseja Kadaka Penalti Moja, mbili kajipanga Burundi wakakosa.
"Kama tulivyoongea jana usiku wachezaji wote mmetimiza kiapo chenu cha jana nami nawaomba kwa muda wenu nitimize kiapo changu kwenu. Mwisho kila mchezo una nyota naomba nimpatie Milioni 10 Ndugu yetu Juma Kaseja kama nyota wangu wa leo," amesema RC Makonda.
Usikubali kupitwa na chochote kile tembelea App hii kila mara kupata Habari zote zinazojiri Tanzania na nje ya Tanzania katika Michezo, Magazeti, Mahusiano, Elimu, Ajira, Video, Audios, Tamthilia na Udaku.