SHIRIKA LA AFYA DUNIANI LAFUNGUKA KUWEPO KWA EBOLA TANZANIA
Baada ya kufanya maboresho katika App yetu sasa tunakuomba ufanye ku update ili kuendelea kupata habari zetu zote pamoja na kutazama mechi live, kusikiliza radio zote za Tanzania na mengine mengi katika ubora zaidi
ILI KU UPDATE BOFYA👉👉👉 HAPA
HAKIKISHA UMEUPDATE
ILI KU UPDATE BOFYA👉👉👉 HAPA
HAKIKISHA UMEUPDATE
Shirika la Afya Duniani ( WHO) na kitengo cha kupambana na magonjwa (CDC) kutoka Marekani, wamethibitisha kuwa Tanzania hakuna mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.
Uthibitisho huo umekuja baada ya Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya, kuruhusu wachukue sampuli za wagonjwa waliodhaniwa kuwa na Ebola na baada ya kupima wamethibitisha kuwa hawakuwa na Ebola.
Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Faustine Ndugulile jana alifanya mazungumzo na Mkurugenzi wa CDC wa Maerekani, Robert Redfield aliyewasili nchini kwa ajili ya kuangalia jinsi Marekani itakavyoweza kushirikiana na Tanzania katika kudhibiti magonjwa ya mlipuko.
Redfied amesema Marekani itaendelea kuisaidia Tanzania katika juhudi zake za kupambana na kudhibiti magonjwa ya mlipuko kupitia’Global Health Security’ huku lengo likiwa ni kuendelea kushirikiana kulinda usalama wa Afya duniani.
Ikumbukwe kuwa mwishoni mwa wiki iliyopita, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alikanusha tetesi za ugonjwa wa Ebola kuwepo nchini na kwamba wagonjwa wawili ambao walihisiwa kuwa na ugonjwa huo vipimo vimeonesha hawana.
Zaidi Na Zaidi Tembelea App Hii Kila Mara , Kila Saa Kupata Habari Zote Zinazojiri Tanzania Na Nje Ya Tanzania Katika Mapenzi Na Mahusiano, Elimu, Ajira, Michezo, Maisha, Magazeti, Videos, Audios, Tamthilia Na Burudani.