YANGA YAUNDA KAMATI YA UHAMASISHAJI
Uongozi wa klabu ya Yanga SC umeunda Kamati ya Uhamasishaji kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya ZESCO United ambao utapigwa Jumamosi ijayo Septemba 14 kwenye uwanja wa Taifa.
Kamati hiyo itakayoongozwa na Mwenyekiti Suma Mwaikenda, wajumbe wake ni Said Mrisho, Clifford Lugora, Abdulmalik Hassan, Dominick Salamba, Hassan Bumbuli, Khamis Dacota, Leavan Maro, Dr David Luhago na Jimmy Msindo.
Wengine ni Jimmy Mafufu, Jacqueline Wolper, Irene Uwoya, Injinia Deo Mutta, Junior Ahmed, King Mwalubadu, Madaraka Malumbo, Hajji Mboto na Miriam Odemba.
Pia wamo Flora Mvungi, Senga, Halima Yahaya ‘Davina’ na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Antony Mavunde, ambaye atakuwa mshauri wa kamati hiyo.
Aidha katika kuonyesha kumuunga mkono kocha Mwinyi Zahera, Septemba 14 viongozi na mashabiki wa Yanga wameaswa 'kutimba' uwanja wa Taifa wakiwa wamevalia 'pensi' kuonyesha kutokubaliana na uamuzi wa TFF kumuadhibu Zahera kwa kuvalia mavazi hayo kwenye mchezo dhidi ya Ruvu Shooting.
Usikubali kupitwa na chochote kile tembelea App hii kila mara kupata Habari zote zinazojiri Tanzania na nje ya Tanzania katika Michezo, Magazeti, Mahusiano, Elimu, Ajira, Video, Audios, Tamthilia na Udaku.