Breaking News

AZAM FC YAENDELEZA WIMBI LA USHINDI LIGI KUU

Baada ya kufanya maboresho katika App yetu sasa tunakuomba ufanye ku update ili kuendelea kupata habari zetu zote pamoja na kutazama mechi live, kusikiliza radio zote za Tanzania na mengine mengi katika ubora zaidi

ILI KU UPDATE BOFYA👉👉👉 HAPA 
HAKIKISHA UMEUPDATE

Klabu ya Azam FC imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa Namungo FC 2-1 usiku wa jana katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam.

Pongezi kwa kiungo mkongwe wa timu hiyo, Frank Raymond Domayo aliyefunga bao la ushindi dakika ya 90 kwa shuti la kipimo kufuatia krosi ya beki Mganda, Nicolas Wadada.

Lakini haukuwa ushindi mwepesi, kwani Azam FC ililazimika kutoka nyuma baada ya kutanguliwa na Namungo FC ambao bao lao lilifunga na mchezaji wao machachari, Lucas Kikoti dakika ya 48.

Mshambuliaji Mzimbabwe, Donald Dondo Ngoma akaisawazishia Azam FC dakika ya 61 akimalizia kazi nzuri ya Wadada pia.
Baada ya mchezo wachezaji wa Namungo FC walimvamia refa Omar Mdoe kutoka Tanga na wasaidizi wake, Kassim Safisha wa Pwani na Abdulaziz Ally wa Arusha kuwalalamikia kabla ya kudhibitiwa na walinzi.
Ligi Kuu itaendelea kesho kwa mchezo mmoja tu, Yanga SC wakiwakaribisha Coastal Union Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam, wakitoka kucheza mechi nne mfululizo bila ushindi, ikitoa sare mbili na kufungwa mbili.

Zaidi Na Zaidi Tembelea App Hii Kila Mara , Kila Saa Kupata Habari Zote Zinazojiri Tanzania Na Nje Ya Tanzania Katika Mapenzi Na Mahusiano, Elimu, Ajira, Michezo, Maisha, Magazeti, Videos, Audios, Tamthilia Na Burudani.