MECHI YA ENGLAND VS BULGARIA YAPELEKEA WATU WANNE KUTIWA MBARONI
Baada ya kufanya maboresho katika App yetu sasa tunakuomba ufanye ku update ili kuendelea kupata habari zetu zote pamoja na kutazama mechi live, kusikiliza radio zote za Tanzania na mengine mengi katika ubora zaidi
ILI KU UPDATE BOFYA👉👉👉 HAPA
HAKIKISHA UMEUPDATE
ILI KU UPDATE BOFYA👉👉👉 HAPA
HAKIKISHA UMEUPDATE
Jeshi la polisi nchini Bulgarian limewakamata watu wanne kwakuwa na mahusiano ya moja kwa moja na mashabiki ambao walikuwa wakitoa kauli za kibaguzi zilizojaa matusi kwenye mchezo wa kufuzu michuano ya Ulaya 2020 baina ya England dhidi ya wenyeji wao Bulgaria uliyopigwa kwenye uwanja wa Sofia.
‘
Kwenye mchezo huo England ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa jumla ya bao 6 – 0 dhidi ya wenyeji wao Bulgaria licha ya kuwa mechi hiyo ilisimamishwa mara mbili katika kipindi cha kwanza kufuatia kauli hizo za kibaguzi zilizokuwa zikitolewa na mashabiki wa timu mwenyeji.
‘European football governing body UEFA’ imeanza taratibu za kuipatia adhabu Bulgaria kufuatia tukio hilo, wakati Rais Aleksander Ceferin akionyesha kutovumilia vitendo vya kibaguzi katika soka.
Na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Bulgaria imesema Jumatano hii kwamba tayari imewakamata watu wanne na msako mkali unaendelea kwa wengine wote wliohusika.
Maneno ya kibaguzi yalikuwa yakisikika hadharani uwanjani kipindi cha kwanza wakati beki wa England, Tyrone Mings akiwa ni miongoni mwa wachezaji waliyokuathirika zaidi na maneno hayo hadi kupelekea kumweleza mwamuzi kutoka Croatia, Ivan Bebek.
Zaidi Na Zaidi Tembelea App Hii Kila Mara , Kila Saa Kupata Habari Zote Zinazojiri Tanzania Na Nje Ya Tanzania Katika Mapenzi Na Mahusiano, Elimu, Ajira, Michezo, Maisha, Magazeti, Videos, Audios, Tamthilia Na Burudani.