Breaking News

SIMBA YABEBA TUZO TATU NDANI YA DAKIKA 360

Baada ya kufanya maboresho katika App yetu sasa tunakuomba ufanye ku update ili kuendelea kupata habari zetu zote pamoja na kutazama mechi live, kusikiliza radio zote za Tanzania na mengine mengi katika ubora zaidi

ILI KU UPDATE BOFYA👉👉👉 HAPA 
HAKIKISHA UMEUPDATE


MABINGWA watetezi Simba, msimu huu mpya wametumia dakika 360 kutwaa tuzo tatu ambazo zinatolewa na Kamati ya Tuzo ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutokana na kufanya vema kwa wachezaji wao pamoja na Kocha Mkuu, Patrick Aussems.

Aussems akiwa kwenye benchi la ufundi ameingoza timu yake kushinda mechi zote nne walizocheza na kwenye mwezi Agosti, mshambuliaji Meddie Kagere aliibuka mchezaji bora akiwashinda Luka Kikoti wa Namungo FC na Seif Karihe wa Lipuli FC.

Mwezi Septemba tena zali liliwaangukia Simba ambapo safari hii walitwaa tuzo zote mbili ikiwa ni ile ya mchezaji bora iliyokwenda kwa Miraj Athuman akiwashinda Meddie Kagere wa Simba na Ismail Kada wa Polisi Tanzania.

Aussems alitwaa tuzo hiyo aliwashinda Abdallah Mohamed ‘Bares’ Kocha Mkuu wa JKT Tanzania pamoja na Adolf Rishard wa Tanzania Prisons.

Ndani ya dakika 360 Simba imejikusanyia tuzo tatu ikiwa ipo kileleni na pointi zake 12 imefungwa mabao mawili pekee mpaka sasa, mchezo wake unaofuata ni dhidi ya Azam FC uwanja wa Uhuru, Octoba 23.

Zaidi Na Zaidi Tembelea App Hii Kila Mara , Kila Saa Kupata Habari Zote Zinazojiri Tanzania Na Nje Ya Tanzania Katika Mapenzi Na Mahusiano, Elimu, Ajira, Michezo, Maisha, Magazeti, Videos, Audios, Tamthilia Na Burudani.