Breaking News

PYRAMIDS YAIPELEKA YANGA CAF

Baada ya kufanya maboresho katika App yetu sasa tunakuomba ufanye ku update ili kuendelea kupata habari zetu zote pamoja na kutazama mechi live, kusikiliza radio zote za Tanzania na mengine mengi katika ubora zaidi

ILI KU UPDATE BOFYA👉👉👉 HAPA 
HAKIKISHA UMEUPDATE


Inaelezwa kuwa uongozi wa klabu ya Pyramids FC ya Misri umetuma malalamiko kwenda Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) ukigomea kitendo cha Yanga kubadilisha uwanja wa kuchezea mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga itamenyana na Pyramids Oktoba 27 kwenye mechi ya raundi ya kwanza ambayo awali ilifahamika itanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam lakini baadaye Yanga wakaamua ichezewe Mwanza kwenye dimba la CCM Kirumba.

Kufuatia mabadiliko ya uwanja huo, imekuwa kama Pyramids wameshtukia na wameamua na taarifa zinasema wametuma malalamiko hayo CAF ili kujua sababu rasmi.

Taarifa zinasema Pyramids wanaona kama ni mbinu za Yanga kuwapoteza kwenye mechi hiyo mpaka imefikia hatua ya kuhoji CAF.

Timu hizo mbili zitakutana katika mechi hiyo ya Play Off ambapo mshindi atafuzu mpaka hatua ya makundi ya mashindano hayo.

Zaidi Na Zaidi Tembelea App Hii Kila Mara , Kila Saa Kupata Habari Zote Zinazojiri Tanzania Na Nje Ya Tanzania Katika Mapenzi Na Mahusiano, Elimu, Ajira, Michezo, Maisha, Magazeti, Videos, Audios, Tamthilia Na Burudani.