Breaking News

SIMBA YALIPA KISASI KWA MASHUJAA FC (MECHI YA KIRAFIKI)

Baada ya kufanya maboresho katika App yetu sasa tunakuomba ufanye ku update ili kuendelea kupata habari zetu zote pamoja na kutazama mechi live, kusikiliza radio zote za Tanzania na mengine mengi katika ubora zaidi

ILI KU UPDATE BOFYA👉👉👉 HAPA 
HAKIKISHA UMEUPDATE

Mchezo wa kirafiki kati ya Mashujaa FC dhidi ya Simba SC uliopigwa katika uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma, umemalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Pamoja na changamoto ya hali isiyoridhisha ya uwanja, Simba iliweza kuwapa burudani wakazi wa mkoa wa Kigoma na maeneo ya jirani ambao walijitokeza kwa wingi kuwashuhudia mabingwa hao wa nchi

Bao pekee la wekundu wa Msimbazi liliwekwa kimiani na kiungo fundi Sharaff Elden Shiboub kwenye dakika ya 57.

Huo ulikuwa mchezo wa kwanza wa Simba katika ziara yake ya Kigoma, ambapo Jumatano ya October 16 itakamilisha ziara yake kwa kumenyana na Aigle Noir ya nchini Burundi.

Zaidi Na Zaidi Tembelea App Hii Kila Mara , Kila Saa Kupata Habari Zote Zinazojiri Tanzania Na Nje Ya Tanzania Katika Mapenzi Na Mahusiano, Elimu, Ajira, Michezo, Maisha, Magazeti, Videos, Audios, Tamthilia Na Burudani.