Breaking News

YANGA SC YACHAPA FRIENDS RANGERS (MECHI YA KIRAFIKI)

Baada ya kufanya maboresho katika App yetu sasa tunakuomba ufanye ku update ili kuendelea kupata habari zetu zote pamoja na kutazama mechi live, kusikiliza radio zote za Tanzania na mengine mengi katika ubora zaidi

ILI KU UPDATE BOFYA👉👉👉 HAPA 
HAKIKISHA UMEUPDATE

KATIKA kujiandaa na mchezo dhidi ya Pyramids FC ya Misri, leo asubuhi Yanga SC imecheza mechi ya kirafiki dhidi ya Friends Rangers ya Daraja la Kwanza na kuibuka na ushindi wa 4-3 Uwanja wa Chuo cha Maafisa wa Jesh la Polisi, Kurasini mjini Dar es Salaam.

Mabao ya Yanga katika mchezo wa leo yamefungwa na wachezaji wa kigeni watupu, washambuliaji Mzambia Maybin Kalengo dakika ya 20 na David Molinga ‘Falcao’ dakika ya 23 na 27 pamoja na kiungo Papy Kabamba Tshishimbi dakika ya 32, wote kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Kwa upande wao, Friends Rangers mabao yao yamefungwa na Lawrence Peter dakika ya 46, Robert Mwaruka dakika ya 86 na Abeid Kisiga dakika ya 89.
 
Yanga watakuwa wenyeji wa Pyramids FC Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza Jumapili ya Oktoba 27, mwaka huu katika mchezo wa kwanza wa mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Bado Pyramids FC hawajataja rasmi Uwanja utakaotumika kwa mchezo wa marudiano Novemba 3, mwaka huu ingawa inafahamika wamekuwa wakitumia Uwanja wa Jeshi la Anga wa Juni 30 mjini Cairo kwa mechi zao za nyumbani.

Yanga imeangukia katika mchujo baada ya kutolewa na Zesco United ya Zambia kwa jumla ya mabao 2-1 kufuatia sare ya 1-1 Dar es Salaam kabla ya kwenda kufungwa 2-1 Ndola.

Katika Raundi ya kwanza, Yanga iliitoa Township Rollers ya Botswana kwa mabao 2-1, ikishinda 1-0 Gaborone baada ya sare ya 1-1 Dar es Salaam. 

Zaidi Na Zaidi Tembelea App Hii Kila Mara , Kila Saa Kupata Habari Zote Zinazojiri Tanzania Na Nje Ya Tanzania Katika Mapenzi Na Mahusiano, Elimu, Ajira, Michezo, Maisha, Magazeti, Videos, Audios, Tamthilia Na Burudani.