Breaking News

WAKENYA WAPOKEA MIILI YA JAMAA NA NDUGU ZAO WALIOKUFA KATIKA AJALI YA NDEGE ETHIOPIAN AIRLINES

Baada ya kufanya maboresho katika App yetu sasa tunakuomba ufanye ku update ili kuendelea kupata habari zetu zote pamoja na kutazama mechi live, kusikiliza radio zote za Tanzania na mengine mengi katika ubora zaidi

ILI KU UPDATE BOFYA👉👉👉 HAPA 
HAKIKISHA UMEUPDATE

Wakenya wamekusanyika kupokea mabaki ya miili ya wapendwa wao waliokufa katika ajali ya ndege ya Ethiopian Airlines Familia za wahanga wa ajali ya ndege ya Ethiopian Airlines iliyoanguka mjini Addis Ababa mwezi Machi na kuwauwa watu wote 157 waliokuwemo ndani ya ndege hiyo wamekusanyika mjini Nairobi kwa ajili ya kupokea miili ya jamaa zao.
Wakenya thelathini na wawili walikufa katika ajali hiyo.
Remains of 32 Kenyans who died in March 10, 2019, Ethiopian air crash arrive at JKIA; to be handed over to respective families.
See Ali 'Mwamvita' Manzu's other Tweets
Awali redio ya kibinafsi nchini Kenya imetuma ujumbe wa Twitter ulioonyesha picha za wahanga wa ajali hiyo, katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jommo Kenyatta mjini Nairobi.
Families of passengers who perished in Ethiopian airline crash at JKIA to receive the remains.
View image on TwitterView image on TwitterView image on TwitterView image on Twitter
See Radio Citizen's other Tweets
Ndege hiyo chapa ET302 kutoka katika mji mkuu wa Ethiopian Addis Ababa kuelekea Nairobi nchini Kenya iliangua muda mfupi baada ya kuondoka.
Vipimo vya vinasaba DNA kuoanisha masalia ya watu 157 waliouawa katika ajali hiyo vilifanyika miezi kadhaa iliyopita baada ya ajali.
Watu kutoka nchi 30 walikuwa wamepanda ndege hiyo huku wengi wao wakiwa ni raia wa Kenya.
Zimekuwa ni siku za huzuni kwa familia za Wakenya 32 waliouawa ambapo watapata fursa kwa mara ya kwanza kutazama masalia ya miili ya wapendwa wao.
Mazishi ya faragha yatafanyika leo Jumatatu , lakini haijawa wazi ikiwa masalia hayo yatatolewa kwa familia zao.
Maafisa nchini Ethiopia wanasema miili mingine ambayo bado haijafahamika itazikwa katika kaburi la kumbukumbu litakalowekwa katika eneo la tukio la ajali hiyo.
People gather at the Ethiopian Airline crash siteHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWatu waliokuwa wamekusanyika kwenye eneo la tukio la ajali ya ndege ya Ethiopian Airline
ndege ya Boeing 737 Max-8 ilianguka miezi sita tu baada ya ndege nyingine ya aina hiyo kuanguka na kuwauwa watu 190 waliokuwemo.
Awali ndugu na jamaa wa wahanga wa ajali hiyo walilalamikia shirika la Boeing kwa kuchelewa kutoa matokeo ya vinasaba ambayo yangesaidia kutambua miili ya wapendwa wao.
Iliripotiwa kuwa miili ya wahanga wa ajali hiyo ilikuwa imeteketea kiasi cha kutotambulika kwa urahisi.
Wakati huo huo ndugu wa watu waliouawa katika ajali ya ndege aina ya Boeing 737 Max iliyopata ajali nchini Indonesia mwaka jana wamekuwa wakidanganywa ili wasipatiwe fidia, wamesema mawakili wao.
Mawakili wao waliiambia BBC kuwa familia nyingi zilishawishiwa kusaini fomu zinazowazuwia kuchukua hatua za kisheria.
Rubani Yared Mulugeta Gatechew aliyefariki katika ajli ya ndege ya Ethiopian Airlines
Image captionRubani Yared Mulugeta Gatechew aliyefariki katika ajli ya ndege ya Ethiopian Airlines
Kipindi cha BBC cha Panorama kiligundua kuwa jamaa wengine wa waathiriwa walisaini makubaliano sawa na hayo baada ya ajali nyingine mbili, zilizowazuwia kuishtaki kampuni ya Boeing katika mahakama za Marekani.
Boeinghaikutoa kauli yoyote juu ya makubaliano hayo.
Abiria wote 189 na wahudumu wa ndge walikufa wakati ndge ya Boeng 737 Max ilipoanguka baharini dakika 13 tu baada ya kuondoka kutoka katika mji mkuu wa Indonesia Jakarta tarehe 29 Octoba 2018.
katika kipindi cha wiki kadhaa, ndugu wa waathiriwa walilipewa fidia na mawakili wa kampuni ya bima

Chanzo BBC.
Zaidi Na Zaidi Tembelea App Hii Kila Mara , Kila Saa Kupata Habari Zote Zinazojiri Tanzania Na Nje Ya Tanzania Katika Mapenzi Na Mahusiano, Elimu, Ajira, Michezo, Maisha, Magazeti, Videos, Audios, Tamthilia Na Burudani.