Breaking News

LUIZ AAHIDI KUIFANYIA RWANDA MAMBO MAKUBWA KWENYE SEKTA YA UTALII

Baada ya kufanya maboresho katika App yetu sasa tunakuomba ufanye ku update ili kuendelea kupata habari zetu zote pamoja na kutazama mechi live, kusikiliza radio zote za Tanzania na mengine mengi katika ubora zaidi

ILI KU UPDATE BOFYA👉👉👉 HAPA 
HAKIKISHA UMEUPDATE

Mchezaji wa klabu ya Arsenal, David Luiz ameahidi kuitangaza Rwanda kimataifa kwenye sekta ya utalii kwa marafiki zake wanaoishi Ulaya na nchini kwao Brazil.Image result for david Luiz in Rwanda
Akiongea na waandishi wa habari wikiendi iliyopita Jijini Kigali nchini Rwanda, David Luiz amesema kuwa atajitahidi kuwashawishi marafiki zake waitembelee nchi hiyo wanapokuwa likizo.
Nimefurahi sana kuwa hapa Rwanda, Tangu siku ya kwanza nafika hapa. Nadhani siku za mbeleni nitarudi tena,“Ameeleza David Luiz na kujibu aliyojionea wakati alipotembelea mbugani.
Tulitembea sana msituni na nimefurahi sana kuwaona sokwe mtu, Nitaenda kuwambia pia rafiki zangu wanaoishi Ulaya na Brazil, kuitembelea Rwanda pindi wanapopata likizo,” – amesema David Luiz.
David Luiz alikuwa nchini Rwanda kwa siku mbili, Kwenye ziara yake ya kikazi kupitia mradi wa kutangaza utalii nchini humo wa Visit Rwanda ambao umesainiwa mwaka jana kati ya Serikali ya Rwanda na klabu hiyo.
Luiz akiwa nchini humo pia alitembelea makumbusho ya mauaji ya kimbari, Hifadhi ya mlima volcano, na kukaribishwa Ikulu na Rais kagame.
Zaidi Na Zaidi Tembelea App Hii Kila Mara , Kila Saa Kupata Habari Zote Zinazojiri Tanzania Na Nje Ya Tanzania Katika Mapenzi Na Mahusiano, Elimu, Ajira, Michezo, Maisha, Magazeti, Videos, Audios, Tamthilia Na Burudani.