Breaking News

BREAKING: NDEGE YA ABIRIA YAANGUKA DR CONGO

Ndege ya abiria iliokuwa ikiwabeba watu 16 imeanguka katika mji wa Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya DR Congo.
Watu walikusanyika katika eneo la mkasa ili kuwasaidia manusura
Gavana wa jimbo la Kivu kaskazini Nzanzu Kasivita Carly amesema kwamba watu wamefariuki lkaini hakutoa idadi kamili .
Ndege hiyo ilianguka juu ya nyumba katika eneo jirani la Mapendo baada ya kushindwa kupaa katika uwanja wa ndege wa mji huo , aliongezea.
Ndege hiyo aina ya Doenier 228 ilikuwa ikimilikiwa na kampuni binafsi ya Busy Bee.
Ilitarajiwa kuelekea Beni yapata kilomita 350 kutoka kaskazini mwa Goma , wakati ilipoanguka dakika moja baada ya kupaa kulingana na chanzo kimoja katika mji wa Goma kilichozungumza na BBC.

: Un crash d'avion serait à la base de plusieurs morts dans le Quartier MAPENDO. Des morts calcinés dans l'avion, et même ceux qui étaient dans le parrage où le crash s'est fait. @luchaRDC @gisele_kaj @TinaSalama2 @pascal_mulegwa @soniarolley @fatshi13
See Ushindi's other Tweets
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE