Breaking News

VIDEO: RAIS MAGUFULI ATOA SIKU 60 KWA TAASISI HIZI

Rais Magufuli ametoa siku 60 kwa mashirika na taasisi zaidi ya 180 za serikali ambazo hazijatoa gawio kufanya hivyo la sivyo bodi ya taasisi hizo zivunjwe. “Waandike barua, kama ni mwenyekiti wa kuteuliwa na mimi siku hiyo sio mwenyekiti tena.”

Rais Magufuli ameongeza “Tuna taasisi na mashirika 266, yaliyoleta gawio ni 79, nawapongeza sana mlioleta, lakini mashirika mengine hayana haja ya kuchangia, na serikali imeweka pale fedha zake Tsh. Tril. 59.6 fedha za Watanzania. Hatuwezi kuendelea kukaa na mashirika ya namna hii, Waziri wa Fedha natoa siku 60 kuanzia leo, wawe wameshakabidhi kwako gawio, wasipo kabidhi kwako gawio bodi zile zijivunje zenyewe.”
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE