Breaking News

KIKOSI CHA KILIMANJARO STARS, MANULA AREJESHWA

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars' Etienne Ndayiragije ameweka hadharani majina ya wachezaji 32 wanaounda kikosi kitakachoshiriki michuano ya CECAFA Challenge Cup ikayaofanyika nchini Uganda.

KIPA namba moja wa timu ya Simba, Aishi Manula amerejeshwa kwenye kikosi cha timu ya taifa, baada ya jana kutajwa kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) kitachoshiriki michuano ya CECAFA Senior Challenge nchini Uganda .

Chini ya kocha wa sasa Etienne Ndayirajige, Manula aliitwa mara moja pekee katika mechi za awali kufuzu CHAN, lakini kuumia kukamuweka pembeni, hakujumuishwa tena Katika mtanange mingine ikiwamo kufuzu Makundi ya awali Kombe la Dunia pamoja na Afcon mechi za awali.

Katika kikosi hicho kipya cha Tanzania Bara wameitwa wachezaji wapya kutoka timu mbalimbali za ligi kuu  ambao ni Juma Abdul (Yanga),Nickson Kibabage (Difaa El Jadid) ,Mwaita Gereza (Kagera Sugar), Abdulimajid Mangalo(Biashara United), Fred Tangalu (Lipuli) na Kikoti Lucas (Namungo).
Wengine ni Yussuf Mhilu (Kagera Sugar), Eliud Ambokile (TP Mazembe), Paul Nonga (Lipuli), Mkandala Cleophace (Tz Prisons) na Zawadi Mauya (Kagera Sugar) .

Wachezaji waliokuwa kwenye kikosi cha hivi karibuni Juma Kaseja (KMC), Matecha Mnata na Kelvin Yondani (Yanga), David Kisu(Gor Mahia), Salum KImenya(TZ Prisons), Bakari Mwamnyeto(Coastal Union)Mohamed Hussein, Miraji Athuman,Jonas Mkude, Muzaru Yassin, Gadiel Michael  na Hassan Dilinuga (Simba).

Wengine ni Shaaban Chilunda, Salum Abubakar Sure Boy na Idd Seleman (Azam) Ditram Nchimbi(Polisi Tanzania), Keklvin John( Football House) na Eliuther Mpepo (Bulidco-Zambia).
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE