Breaking News

MATOKEO YA YANGA VS ALLIANCE FC

KIKOSI cha Yanga kimeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuwachapa wenyeji, Alliance FC  2-1 jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.

Kwa ushindi huo, Yanga SC mabingwa mara nyingi zaidi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara, wanafikisha pointi 16 katika mchezo wa saba na kupanda hadi nafasi ya 12 kutoka ya 15.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Emmanuel Mwandemwa aliyesaidiwa na Abdulaziz Ally wote wa Arusha na Charles Simon wa Dodoma, hadi mapumzuko Yanga SC walikuwa mbele kwa bao 1-0.

Bao hilo lilifungwa na mshambuliaji wake mpya kutoka Rwanda, Patrick Sibomana dakika ya 25 akimalizia mpira uliorudi baada ya kuokolewa kwa pigo la kichwa na Nahodha Mkongo Papy Kabamba Tshishimbi aliyeunganisha krosi ya beki wa kushoto, Jaffar Mohamed.

Lakini dakika 10 tu baada ya kuanza kipindi cha pili, Alliance FC ikasawazisha bao hilo kupitia kwa mshambuliaji wake, Juma Nyangi akimalizia pasi ya David Richard.

Na ndipo mshambuliaji mpya, David Molinga Ndama ‘Falcao’ alipoibuka shujaa kwa bao lake la ushindo dakka ya 72 akimalizia pais ya kiungo Deus Kaseke.

Mfungaji wa bao la kwanza, Sibomana hakumaliza mchezo baada ya kuumia na kushindwa kuendelea, nafasi yake ikichukuliwa na kiungo Raphael Daudi dakika ya 90 na ushei.

Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, Kagera Sugar imelazimishwa sare ya 0-0 na Ndanda FC Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE