KERR ATAJWA SIMBA SC
Aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa klabu ya Simba, Dylan Kerr, amesema hana tatizo na wekundu hao wa Msimbazi endapo watamwitaji.
Kerr ambaye kwa sasa yuko England ameibuka na kusema kama Simba wanahitaji huduma yake atakuwa tayari kukaa mezani ili wazungumze.
Kocha aliwahi kuifundisha Simba akiwa sambamba na Seleman Matola kama msaidizi ambaye kwa sasa anaifundisha Polisi Tanzania.
Kerr aliondoshwa Simba kufuatia kuharibu katika michuano ya Mapinduzi huko Zanzibar miaka kadhaa iliyopita.
Ukiachana na Kerr ambaye alikuwa rafiki wa karibu zaidi na Abdi Banda anayekipiga Afrika Kusini, Simba inatajwa kuzungumza na Goran Kopunovic na hii ni kufuatia uvumi uliopo kuwa Patrick Aussems anaweza akaondoka.
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE