SITA WAPIGWA CHINI YANGA, WATANO WAPYA WATAJWA
Wakati mabingwa wazamani wa Ligi Kuu Yanga, ikianza kufanya vizuri katika michuano hiyo msimu huu, kinachofuata sasa ni kuimarisha kikosi ili iweze kutimiza ahadi ya kurudisha ubingwa unaotetewa na wapinzani wao Simba. Imeelezwa.
Taarifa imeeleza kuwa katika kufanikisha hilo, moja ya mikakati ambayo tayari imeiva ni kuhakikisha timu inasajili wachezaji wenye uwezo wa kufikia malengo yao na pia kupiga panga wale wanaoonekana kuwa mizigo ndani ya kikosi.
Habari zinasema kuwa, zoezi hilo linatarajia kufanywa wakati wa usajili wa dirisha dogo linalotarajiwa kufunguliwa Desemba 16 mwaka huu hadi Januari 15 mwakani.
Tayari baadhi ya majina ya kutoka na kuingia yameshatua mezani kwa Mwenyekiti wa klabu hiyo Dkt Mshindo Msolla, vilevile kamati ya ufundi ya klabu hiyo imekuwa ikiendelea kufanya upembuzi ili kubaini wachezaji wasiofaa kuendelea kuwepo, zoezi linalofanywa katika mechi mbalimbali ikiwemo ya juzi dhidi ya JKT Tanzania.
Katika mchezo huo ambao ulichezwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, licha ya Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya maafande hao, kocha Boniface Mkwasa alikiri kuwa na mapungufu mengi katika kikosi chake.
Mapungufu hayo hayataishia kuyafanyia kazi mazoezini bali kuna mashine mpya za kazi zitasajiliwa ili kurejesha heshima ya Yanga kuwa ya makombe kama ilivyokuwa huko nyuma.
Kiongozi wa juu wa Kamati ya Utendaji ya Wanajangwani hao ambaye hakutaka jina lake liandikwe aliweka wazi mipango yao ya usajili, pamoja na nyota watakaofungashiwa virago.
"Tunaachana na wachezaji sita, sitaweza kukutajia majina, lakini kukusadia ni kwamba wa kigeni wawili wanacheza safu ya ushambuliaji na wazawa watatu.
"Kwa haraka haraka wanaoingia ni watatu, beki wa kushoto mmoja, beki wa kati na kiungo mshambuliaji mmoja na hao wawili bado tunawawindai," alisema.
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE