MANARA ATAMBULISHA KITENGO CHAKE CHA HABARI SIMBA
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Haji Sunday Manara ametambulisha watendaji katika kitengo cha Habari na Mawasiliano klabu ya Simba.
Manara amewataja Jacob Gamaly na Rabbi Hume kama maafisa anaofanya nao kazi katika kitengo hicho.
"Tuna kitengo imara sana cha mitandao ya kijamii ambacho kinaongozwa na Rabbi Humwe"
"Yeye ndio husimamia mitandao yetu ya kijamii chini ya uratibu wangu," amesema Manara
"Mwingine ni Jacob Gamaly, kijana wangu aliyekuwa msaidizi binafsi katika ofisi yangu na sasa amepanda cheo na kuwa msaidizi wa masuala ya habari na masoko"
"Pia yupo Abbas Said ambaye ndiye Mratibu wa klabu yetu"
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE