Breaking News

MO AINGIZA BILIONI 20 ZA UWEKEZAJI SIMBA


Kaimu Mwenyekiti wa klabu ya Simba Mwina Kaduguda amesema kuwa Mwekezaji wa klabu hiyo Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' ameshaingiza kiasi cha Tsh Bilioni 20 za uwekezaji kwenye akaunti ya klabu ya Simba.

Kukamilika kwa hatua hiyo ni ishara kwamba mchakato umekamilika ambapo hatua itakayofuata ni uuzwaji wa hisa asilimia 51 kwa Wanachama.

Aidha Mo anamiliki hisa asilimia 49 ambazo thamani yake ni Tsh Bilioni 20.


Mchakato wa fedha hizo kuingizwa kwenye akaunti ya Simba ulichelewa kutokana na kutokamilika kwa baadhi ya masuala ya kisheria.
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE