Breaking News

MATOKEO YA SIMBA VS KMC, MECHI YA KIRAFIKI

TIMU ya Simba SC leo imechapwa 2-1 na wapinzani wao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, KMC katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Mussa Gabriel aliyesaidiwa na Innocent Mwalutanile na Hassan Buhanza baada ya dakika 45 ngumu za kipindi cha kwanza, milango ikafunguka kipindi cha pili.

Mabao ya KMC yamefungwa na kiungo Kenny Ally Mwambungu dakika ya 58 na 68, wakati la Simba limefungwa na Ibrahim Ajibu kwa penalti dakika ya 90 na ushei baada ya kiungo Mbrazil, Gerson Fraga ‘Viera’ kuangushwa kwenye boksi. 

KMC ilikuwa inacheza mechi ya kwanza tangu imefukuze kocha wake Mganda, Jackson Mayanga na leo ikiwa chini ya kaimu kocha Mkuu, Mrage Kabange imepata ushindi. 
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE