MFAHAMU KINDA WA NIGERIA CHUKWUEZE ANAYEIPA KIBURI VILLARREAL PALE LA LIGA
Ni kawaida kila ligi kuwa na wachezaji vijana, wapo wenye mwanzo mzuri na wengine hushindwa kuonyesha uwezo wao wakiwa katika hatua hizo za awali, hilo ni tofauti na kinda wa Nigeria, Samuel Chukwueze amekuwa moto wa kuotea mbali pale La Liga akiwa anaitumikia klabu yake ya Villarreal.
Samuel Chukwueze mwenye umri wa miaka 19 pekee ameanza kuwa mchezaji muhimu nani ya timu yake ya Villarreal kutokana na uwezo wake wa kucheka na nyavu.
Kinda huyo anayeitumikia vyema uzi wake wa rangi ya Njano amekuwa na msimu wenye mafanikio makubwa hasa ikikumbukwa pale alipoanza kuzinyanyasa nyavu za La Liga Novemba 4 2018 dhidi ya Levante akipachika bao lake na kuwazawadia waajiri wake hao.
Ni vigumu kusahau namna alivyofunga bao la kwanza ndani ya La Liga alipotuwa tu, Novemba 11 wakati alipowanyanyasa walinzi kabla ya kumpa shughuli ya kufanya mlinda lango wa klabu ya Rayo Vallecano, Dimitrievski ambapo mwisho alishudia mpira ukienda nyavuni na kukosa cha kufanya.
Mnigeria huyo amekuwa ni mtu wa kuweka rekodi, akiwa ndani ya uzi wa njano mwaka 2018 aliweza kuifungia bao klabu yake ikiwa inawania kusonga mbele zaidi kwenye michuano ya Europa League hatua ya makundi dhidi Spartak Moscow ambapo walifanikiwa kutoka na ushindi wa mabao 2 – 0.
Mwiba huu ambao sasa umekuwa na jina pale La Liga, ni mzaliwa wa Mei 22 mwaka 1999 pale Abia State, Nigeria. Licha ya familia yake kumtaka kuwa bize zaidi na kitabu lakini binafsi alikuwa akiupenda mpira zaidi.
Kijana huyu, Chukwueze alianza maisha yake ya soka pale kwenye Diamond Football Academy na uwezo wake ulianza kuonekana alipokuwa akitumikia timu yake ya taifa ya Nigeria kwa vijana walio na umri chini ya miaka 17 mwaka 2015 ambapo waliweza kutwaa kombe la dunia kwa wachezaji wa umri huo huku akifunga mabao matatu kati ya matano waliyofunga mbele ya Chile na matokeo kumaliza kwa 5 – 1.
Mnamo mwaka 2017 ndipo akapa fursa ya kujiunga na Villarreal ngazi ya vijana lakini kutokana na uwezo wake ambao alikuwa akiuonyesha basi alijikutana akipandishwa mpaka timu C kisha B na kocha akaona kipaji chake bila kujali umri aliyonao akajikuta akivutiwanaye na kumpa nafasi nndani ya kikosi cha watu wazima.
Mwenendo wa Chukwueze ndani ya La Liga unafananishwa mno na mchezaji wa zamani wa Nigeria na klabu ya Real Madrid, Christopher Ohen. Mshambuliaji huyu wazamani wa Madrid alifanya makubwa sana zama zake miaka hiyo ya 1990 akifanikiwa kufunga jumla ya mabao 48 ndani ya michezo 117 aliyopata kucheza ambapo ilifamnya kuwa mchezaji wa tatu mwenye magoli mengi kutokea Afrika kwenye historia ya ligi hiyo ya Hispania.
Samuel Chukwueze kwa sasa ameingizwa kwenye majukumu ya timu ya taifa ya Nigeria, na Novemba iliyopita akiwa kwenye kikosi hicho waliweza kutoka sare tasa ya bila kufungana 0 – 0 dhidi ya Uganda. Kwa sasa kijana huyo anaangazia zaidi namna gani ataweza kufanya vyema zaidi kwenye klabu yake ya Villarreal hali itakayopelekea kuwa tegemezi, huku msimu wa mwaka 2018/19 ukiwa mgumu kwa upande wake licha ya hapo jana kuipatia bao pekee klabu yake dakika ya 59 wa wakipoteza kwa magoli 3 – 1 dhidi ya Celta Vigo.
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE